Huduma za Biashara

Imewekwa: 11/09/2018

FURSA YA KUUZA BIDHAA YA KUNGUMANGA NA KAKAO

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inapenda kuwataarifu wafanyabiashara wa kungumanga na kakao kwamba tumepokea mahitaji ya kununua bidhaa hizo kutoka Pretoria, Afrika Kusini na India.

Hivyo Mamlaka inaomba wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza kuchangamkia fursa ya Pretoria, Afrika Kusini na India, kwa hatua zaidi jaza fomu hapa.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa barua pepe info@tantrade.go.tz au kwa namba ya simu 0735 510907 au 0735 647165