Habari

Imewekwa: 22/01/2019

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inawaalika Wadau wote wa Zao la Muhogo nchini kushiriki Mkutano Maalum wenye lengo la kujadili maendeleo ya upatikanaji wa fursa za masoko kwa zao hilo. Kikao kitafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa TanTrade, uliopo Uwanja wa Mwl. J.K. Nyerere, Barabara ya Kilwa - Dar es Salaam tarehe 28 Januari, 2019 kuanzia saa 3.30 asubuhi.

Tafadhali thibitisha ushiriki wako kwa Bw. John Fwalo kupitia simu namba 0767 285 252 au barua pepe: john.fwalo@tantrade.go.tz kabla ya tarehe 25 Januari, 2019.