Habari

Imewekwa: 13/10/2018

​ULEGA; ONGEZENI UZALISHAJI WA KUKU

​ULEGA; ONGEZENI UZALISHAJI WA KUKU

Serikali imewataka Wazalishaji wa kuku na ndege wafugwao kuongeza uzalishaji ili kukidhi uhitaji wa soko uliopo nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega katika Maonesho na Semina ya kuku na ndege wafugwao iliofanyika leo jiji Dar es Salaam katika Uwanja wa Mwl.J.K Nyerere, barabara ya kilwa.
Ambapo amewetaka wazalishaji hao kuitumia vyema fursa iliopo ya uhitaji wa kuku nchini ambayo imetokana na serikali kupiga marufuku uingizwaji nchini wa kuku na ndege wafugwao na mazao yake kutokana na kuwepo kwa tishio la mafua ya ndege.
‘’sisi tumeweka zuio la kutoingiza ndege wafugwao na mazao yake kutokana na tishio la mafua ya ndege,sasa nyie wafugaji itumieni vyema fursa hii kwa kuhakikisha mnazalisha zaidi kuku’’ Alisema Ulega
Ulega ameongeza kuwa kiwango cha ufagaji na idadi ya kuku tulionao bado hakiridhishi hivyo aliwataka wafugaji hao kuongeza uzalishaji na kuacha kufikiria kuwa wataagiza kuku kutoka nje kwa ajili ya soko la ndani.
Kwa upande mwingine Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega ameziagiza Halmashauri nchini kutafakari kujenga maeneo mahususi ambayo yatatumika kuchinja kuku na ndege wengine wafugwao,ambapo hatua hiyo itawavutia wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika mashamba ya kuku.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) Bw.Edwin Rutageruka ameseman TanTrade itawatengea wazalishaji wa kuku na ndege wafugwao eneo maalumu katika Maonesho ya Viwanda vya Tanzania yanayotarajia kuanza tarehe 5 hadi tarehe 9 Desemba,2018 katika Uwanja wa Mwl.J.K Nyerere,barabara ya Kilwa-Dar es Salaam ili waweze kutangaza Viwanda vyao.
Pia amewakaribisha Wafanyabiashara wote (Wadogo, wa Kati na Wakubwa) kushiriki bure “bila kiingilio” Soko la SABASABA kwa ajili ya kuuza bidhaa zao siku ya Jumamosi tarehe 13 Oktoba, 2018 na Jumapili tarehe 14 Oktoba, 2018 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K. Nyerere, Barabara ya Kilwa-Dar es Salaam.