Habari

Imewekwa: 01/04/2019

USHIRIKI KATIKA MIKUTANO YA KIBIASHARA (B2B) KWENYE MAONESHO YA 43 YA DITF

USHIRIKI KATIKA MIKUTANO YA KIBIASHARA (B2B) KWENYE MAONESHO YA 43 YA DITF

Dar es Salaam, Aprili 1, 2019.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inapenda kuwataarifu Jumuiya ya wafanyabiashara na wananchi wote kuwa, inaandaa Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), yanayotarajiwa kuanza tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2019 kwenye Uwanja wa Mwl J.K.Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

Katika Maonesho hayo, kutakuwa na mikutano ya kibiashara (B2B) kwa Sekta ya Kilimo katika bidhaa mbalimbali, ufungashaji kwa bidhaa za kilimo na mashine za kilimo ili kuwa na masoko endelevu kwa maendeleo ya Viwanda na ukuaji wa uchumi. Aidha, Wafanyabiashara na Wazalishaji watapata fursa ya kukutanishwa na wanunuzi wa bidhaa zao kutoka ndani na nje ya nchi

Ili kushiriki katika mikutano hii, tafadhali pakua fomu kupitia Hapa www.tantrade.go.tz na kuiwasilisha kwa barua pepe info@tantrade.go.tz au norah.mishili@tantrade.go.tz. Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu kwa namba 0755 383575 (Bi Norah Mishili).