Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

''NJOONI MFANYE BIASHARA TANZANIA KUNA MASOKO YA UHAKIKA", ASEMA WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA KWENYE MAONESHO YA SABASABA 2025.

  • July 13, 2025

13 JULAI, 2025.


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaakikishia wageni kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni kuja kufanya biashara na  kuwekaza Tanzania kwa maana masoko ya huwakika yapo Tanzania. Aidha Waziri Mkuu ametoa rai kwa taasisi zote zinazojihusisha na biashara kutafuta masoko ya Kimataifa Kwa lengo la kuongeza ushindani katika Biashara, pia Waziri Mkuu amesisitiza matumizi ya nembo yetu ya taifa ya "Made in Tanzania" kwenye bidhaa na huduma zinazozaliswa nyumbani Tanzania. Aidha Waziri Mkuu ametoa rai kwa wazalishaji wote kuzitangaza bidhaa na huduma za Tanzania kwa kutumia vyombo vya Habari, mtandao ya kijamii nk. Ameainisha hayo kwenye siku ya kufunga kwa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025, katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.