Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

PONGEZI WATUMISHI BORA TANTRADE MWAKA 2024-2025

  • June 19, 2025


18 Juni 2025.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade imefanya hafla fupi ya kuwapongeza Watumishi bora wa mwaka 2024/2025 kwa kuwapatia zawadi ya fedha taslim pamoja na vyeti kwa lengo la kuwapa motisha kwa kujituma na nidhamu kazini.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bi. Latifa M. Khamis ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa Watumishi wengine wa Mamlaka hiyo kuzingatia mshikamano, maadili na kufanya kazi kwa bidii huku wakizingatia njia sahihi za mawasiliano katika taasisi.
Hafla hii fupi imefanyika leo katika Ofisi za TanTrade zilizopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.