Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MKOA WA DAR ES SALAAM WATUMIA JUKWAA LA MAONESHO YA SABASABA 2025, KUTANGAZA FURSA ZILIZOPO DAR ES SALAAM.

  • July 10, 2025

10 JULAI, 2025.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa M. Khamis  ametoa rai kwa Watanzania kuja kwenye Maonesho ya Sabasaba bila kusita wakati akiwalisha kwenye siku maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, inayofanyika kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Dar es Salaam Sabasaba 2025. Siku hii ya Dar es Salaam inalenga kuangazia fursa za kibiashara na uwekezajı zilizopo katika Mkoa wa Dar es Salaam. Dar es Salaam day imewakutanisha wafanyabiashara kutoka wilaya zote na wadau mbalimbali wa biashara na uwekezajı. Maonesho ya Sabasaba yamebeba kauli mbiu inayosema " Maonesho ya Biashara ya Kimataifa SABASABA fahari ya Tanzania".