Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

DG. TANTRADE AWAKARIBISHA WANAFUNZI WA CBE KATIKA VIWANJA VYA MWL. NYERERE

  • November 21, 2025

20 Novemba, 2025

Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Dkt. Latifa M. Khamis, amewapongeza wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa kuchagua kujiunga na chuo hicho mahiri kinachotoa mafunzo ya taaluma mbalimbali za biashara.

Akizungumza na wanachuo hao, Dkt. Latifa aliwasihi kuwa na nidhamu, kujituma katika masomo, na kujiepusha na makundi au ushawishi usiofaa ambao unaweza kuhatarisha mustakabali wao wa kitaaluma.

Aidha, alieleza kuwa uwepo wa chuo hicho ndani ya maeneo ya TanTrade ni fursa adhimu kwa wanafunzi hao, kwani TanTrade ni taasisi ya serikali inayosimamia maendeleo ya biashara nchini  hivyo wana nafasi ya kujifunza kwa vitendo kupitia ushirikiano wa karibu na sekta ya biashara