Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MILANGO YA UKUZAJI BIASHARA KIMATAIFA YAENDELEA KUFUNGULIWA

  • December 11, 2024

10, Desemba 2024.

___

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Bi. Latifa M Khamis leo amezungumza na wawakilishi wa Televisheni ya CNBC na kujadili maswala mbalimbali kuhusu Biashara ikiwemo namna jinsi ambavyo watashirikiana na Mamlaka katika kutangaza soko la Tanzania na bidhaa zinazozalishwa Tanzania kimataifa.

Aidha Televisheni ya CNBC na TanTrade pia watashirikiana kutangaza kikamilifu maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba, yatakayofanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 13 Julai 2025