KILA KITU SHWARI MAANDALIZI YA SABASABA 2025 MSIMU WA 49.
- June 18, 2025

18 Juni, 2025.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 imeketi na kuangazia maeneo mbalimbali ya Maonesho ya Sabasaba 2025. Kamati hii inalenga kuboresha zaidi usimamizi kwa kutoa huduma za kiusalama kwa wanamaonesho, watembeleaji na mali zao katika kipindi chote cha maonesho, Maonesho haya ya Biashara ya Kimataifa yataanza tarehe 28 Juni na kutamatika 13 Julai 2025 huku yakihusisha sekta mbalimbali kama vile Biashara, Utalii, Kilimo, Afya, Elimu, Usafirishaji, Huduma za kibenki, Bima, na maswala mbalimbali ya kijamii.