Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MAANDALIZI YAKO VYEMA KUELEKEA MSIMU WA 49 WA MAONESHO YA SABASABA 2025.

  • June 20, 2025

19 Juni, 2025.

Kamati ya maandalizi ya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam  Sabasaba 2025, imekutana tena leo nakufanya tathmini ya maandalizi ya Maonesho hayo makubwa zaidi Afrika Mashariki yanayohusisha sekta mbalimbali kama vile Elimu, Miundombinu, Ujenzi, Biashara, Kilimo, Nishati na Madini, Maji na nyinginezo. Maonesho haya ya msimu wa 49 yatahusisha ushiriki wa nchi mbalimbali kama vile India, China, Russia, Egypt, Korea, Iran, Uganda, Kenya nk. Maonesho yataanza rasmi tarehe 28 Juni na kutamatika tarehe 13 Julai, 2025.
Kamati hii imeketi leo katika Ofisi za TanTrade zilizopo kiwanja cha Mwl Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.