BANDA LA MADE IN TANZANIA LAWAVUTIA WENGI KWENYE MKUTANO WA SADC WA KUIMARISHA ULINZI, SIASA NA USALAMA.
- July 21, 2025
21 JULAI, 2025.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) katika kutekeleza moja ya jukumu lake madhubuti la kuhamasisha matumizi ya chapa ya Taifa ya "Made in Tanzania" kwenye bidhaa na huduma zinazozalishwa na Watanzania, inaratibu banda katika mkutano wa hamasa ya siasa, ulinzi kwa nchi za SADC ambapo Tanzania ni nchi mwanachama, kupitia banda hilo wageni wanapata fursa ya kuona, kujifunza na kununua bidhaa mbalimbali za Kitanzania. Banda la Made in Tanzania linakutanisha wajasiriamali wadogo, wakati na wakubwa kutoka sekta mbalimbali hususan bidhaa za kibiashara kama vile, kahawa, chai, batiki viungo nk. Mkutano huu unafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere International Conversation Center (JNICC), Jijini Dar es Salaam.