PROGRAMU YA URITHI WETU YA TANTRADE YAWATEMBEZA WANAFUNZI KWENYE MIRADI MBALIMBALI YA SERIKALI.
- July 4, 2025
3 JULAI, 2025
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade katika kutekeleza majukumu yake ya uratibu wa Maonesho ya Sabasaba imekua na programu ya wanafunzi inayofahamika kwa Jina la "URITHI WETU" ambayo huwaleta wanafunzi mbalimbali kutoka mikoa ya nje ya Dar es Salaam kwa lengo kutembelea Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam huku wakijifunza maswala mbalimbali na kutambua miradi ya kimkakati ya Serikali, wanafunzi waliotembelea Maonesho ya Sabasaba leo, walipata fursa ya kupelekwa kwenye mradi wa treni ya mwendo kasi (SGR) kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali na kuiona treni hiyo kwa uhalisia.