Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

KAZI YA MAANDALIZI IENDELEE, SABASABA 2025 MSIMU WA 49.

  • June 21, 2025

20 Juni, 2025.

Dtk. Suleiman Serera Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Bi Latifa M. Khamis Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade wamezuru maandalizi ya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 ambapo zimebaki siku chache kufikia ufunguzi wake.

Maonesho haya ya Biashara ya Kimataifa yataanza tarehe 28 Juni na kutamatika tarehe 13 Julai 2025 katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere (Sabasaba Grounds) barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.