TANTRADE YAPONGEZWA KWA KUFANIKISHA MASOKO YA BIDHAA NA HUDUMA ZA TANZANIA
- November 29, 2025
28 Novemba 2025.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith S. Kapinga (Mb) ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwakua mstari wa mbele katika utafutaji wa masoko kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa nyumbani Tanzania kupitia Maonesho ya ndani na nje, misafara ya biashara wanayoiratibu.
Aidha Waziri Kapinga ametoa maelekezo kwa Mamlaka kuhakikisha, mifumo inasomana na taarifa za biashara na masoko zinawafikia wadau wa biashara kwa usahihi na kwa wakati ilikukuza na kuendeleza maendeleo ya biashara nchini, Mhe. Waziri ameainisha hayo alipotembelea Ofisi za TanTrade zilizopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam wakati akifanya ziara za taasisi anazozisimamia.