Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI UZINDUZI WA NJIA MPYA YA AIR TANZANIA KUTOKA DAR KWENDA JIJINI LAGOS

  • September 26, 2025

Lagos, Nigeria
22 Sept, 2025

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) imeshiriki katika uzinduzi wa njia mpya ya ndege ya moja kwa moja ya Air Tanzania kutoka Dar es Salaam kwenda Jijini Lagos utakaopunguza muda wa Safari na kuwezesha Wafanyabiashara kuingia katika masoko mapya ya biashara pamoja na kuangazia fursa za masoko katika sekta mbalimbali ikiwemo mkonge, ngozi, chai, karafuu na kuangazia kuwezesha usafirishaji wa bidhaa kwa haraka baina ya nchi zote mbili.

Aidha, kupitia ziara hiyo, TanTrade imefanya kikao na Lagos Chamber of Commerce and Industry (LCCI) ambapo akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade Dkt Latifa Mohamed Khamis, 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara alikutana na Mkurugenzi Mkuu wa LCCI Dkt. Chinyere Almona ofisini kwake na kufanya majadiliano ya namna Taasisi hizo mbili zitakavyoweza kushirikiana.