TANZANIA NA INDIA KUIMARISHA MISULI YA MAENDELEO YA BIASHARA. (Siku ya Haryana INDIA SABASABA 2025.)
- July 11, 2025
11 JULAI, 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa M. Khamis aaidi kuendelea vyema ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na India. Biashara baina nchi hizo mbili zinahusisha sekta mbalimbali kama vile, Madawa, Afya, Viwanda, Chakula, Maghala, teknolojia, elimu, kilimo. Wafanyabiashara kutoka taifa la Haryana wamekua wakishiriki Maonesho ya Biashara ya Kimataifa SABASABA, kwa mara tatu mfululizo, na wataendelea kushiriki Sabasaba kwani kwao imekua fursa kubwa kwa wao kukutana na wafananya biashara wa Kitanzania na kutoka mataifa mengine. Siku ya Haryana India imefanyika katika Ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa (Dome) uliopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere Sabasaba Grounds barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.