MKUTANO WA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA NA UMOJA WA NCHI ZA FALME ZA KIARABU (UAE) WAFANA
- December 11, 2024
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) leo imekutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu katika kikao cha Biashara kilichofanyika Hoteli ya Hilton, Dubai.
Kikao hiki kilichofunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo(Mb.) kimelenga katika kuwatafutia wafanyabiashara wa Tanzania masoko ya nje na kuwaunganisha na fursa za Uwekezaji kutoka Nchi za Falme za Kiarabu.
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa M. Khamis alihudhuria Mkutano huu wa Kibiashara na kuainisha fursa mbalimbali za Biashara zinazopatikana Tanzania na pia alichukua fursa hiyo kuwakaribisha wadau kwenye maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yatakayofanyika kuanzia Tar 28 Juni hadi 13 Julai 2025.