MKATABA WA ENEO HURU LA BIASHARA LA AFRIKA (AfCFTA) KUTATUA CHANGAMOTO ZA MASOKO AFRIKA.
- July 24, 2025
24 JULAI, 2025.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ikiwa kama taasisi teule ya kusimamia na kukuza Biashara nchini imeshiriki kikamilifu katika mkakati wa utekelezaji wa eneo huru la biashara la Afrika.
Mkakati wa utekelezaji wa eneo huru la biashara la Afrika unalenga kutatua changamoto za masoko kwa bidhaa za Tanzania kwenye masoko ya Afrika ambapo mkakati huu unaenda kuleta faida kadha wa kadha ikiwemo kuchagiza ukuaji viwanda, kuimarisha ushirikiano wa biashara katika nchi za Afrika, kuongeza ajira, kuondoa vikwazo na ushuru kwenye biashara, kuongeza ajira, kupunguza umasikini, na kuwainua wajasiriamali wadogo. Kupitia mkakati huu tayari Tanzania imeshauza kahawa Algeria na bidhaa nyingine nyingi kwenye nchi mbalimbali Afrika.