WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAJIPANGA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NCHINI.
- December 19, 2025
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith S. Kapinga (Mb) kupitia Idara ya Habari Maelezo ameainisha mpango wa Wizara yake wa kuboresha mazingira ya Biashara kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia, kuboresha ubora wa bidhaa zinazoingia sokoni, kutumia kikamilifu majukwaa mbalimbali ya masoko kama vile soko huru la Afrika Mashariki, Masoko ya Kidigitali (Biashara Mtandao).
Aidha Waziri Kapinga amewahakikishia wafanyabiashara hususan Vijana ya kwamba Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mikopo, kulinda biashara za wazawa, elimu, ajira, mafunzo, kuendeleza ubunifu wa teknolojia kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za umma na binafsi. Ameainisha hayo wakati akiwasilisha maazimio hayo kupitia Idara ya Habari Maelezo.