Habari

Imewekwa: 22/02/2020

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inapenda kuwataarifu wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME’s) wanaozalisha bidhaa za Tanzania kuwa waandaji wa Maonesho ya Dunia ya mwaka 2020 kutoka nchi ya Falme za Kiarabu (EXPO 2020 Dubai) imefungua mfumo wa usajili wa wafanyabiashara kwenye soko la mtandao.

Lengo la mfumo huo ni kutoa fursa ya kuwaunganisha wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nje ya mipaka yao kuuza, kutangaza bidhaa, kufahamiana pamoja na kupeana taarifa za biashara kupitia Mtandao huo . Soko la mtandao ni jukwaa lenye nguvu ya kupata bidhaa na huduma zenye ubora zaidi pamoja na mawazo mapya yenye ubunifu yaliyoendelezwa na wafanyabiashara kutoka sekta ndogo na kati ulimwenguni.

Mfumo huo utawezesha wanunuzi na wauzaji kutafuta na kugundua wadau wao sehemu yoyote duniani na kuwachuja kabla ya kuingia kwenye mfumo wao wa ndani wa kutoa zabuni nje ya mfumo huo uliowekwa na waandaji wa Maonesho ya dunia.

Ili kujisajili, tafadhali tembelea tovuti yetu yenye anuani www.tantrade.go.tz na kubofya linki iitwayo “Sajili Biashara yako-Expo 2020”. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0757 240199 au tembelea ofisi zetu zilizopo katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere barabara ya Kilwa.

Imetolewa na;

Theresa H. Chilambo

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano