Habari

Imewekwa: 09/03/2020

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inapenda kuwakaribisha Waandaaji wa Maonesho, Misafara ya Kibiashara, Wamiliki wa Kumbi za Maonesho, Wizara,Taasisi za Umma na Binafsi zinazohusika na Maswala ya Biashara pamoja na wadau wote kwa ujumla kushiriki Mkutano wa Wadau ulioandaliwa kwa lengo la kupokea Maoni kuhusiana na Kanuni Mpya za Sheria ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, 2019 utakaofanyika katika Ofisi ya Wizara ya Biashara na Viwanda - Mazizini Zanzibar tarehe 12 Machi,2020 Saa 3:00 asubuhi.

Ili kuthibitisha ushiriki wako, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe tahir.ahmed@tantrade.go.tz au info@tantrade.go.tz au kwa simu namba: +255 773 200 735 Bw.Tahir Ahmed.

Imetolewa na;

Theresa H. Chilambo

MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO NA MAWASILIANO